TUKUJUZE MEDIA

TUKUJUZE MEDIA
TUKUJUZE ONLINE MEDIA

Breaking News

Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari ahimiza walimu kupewa elimu kuwasaidia wanafunzi.

May be an image of 1 personMkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari bi Asya Iddi Issa amesema ni jambo zuri kwa walimu kupata Elimu ili waweze kuwasaidia Wanafunzi kupata ujuzi utakaowasaidia kujiendeleza kimaisha mara bada ya kumaliza Skuli.
 
Amesema hayo wakati alipotembelea walimu waliojiunga na darasa la ziada la sanaa( fine art) katika Skuli ya Mwanakwerekwe "C" Sekondari Mjini Unguja amesema, Fani ya auwalimu ni kazi ya wito hivyo kujitolea kujiunga na darasa hilo kutawaongezea ujuzi ambao utakuwa na manufaa kwao na kwa Wanafunzi.
 
Amesema uamuzi wa walimu hao kuweka siku maalumu ya kujengeana uwezo wa taaluma hiyo ni suala la kupigiwa mfano na linawashajihisha walimu kuhakikisha wanatafuta fani hiyo ili nao waweze kuwasaidia na wengine.
 
Amesema somo hilo litakapo tiliwa mkazo litainua vipaji vingi vya wanafunzi katika sana ambavyo vimejificha hasa kwa skuli zao.
 
Amesema somo hilo linasomeshwa hadi Wanafunzi wenye mahitaji maalum Kwani litawasaidia wanafunzi hao kuonesha uwezo wao wa kuitumia sanaa katika kujikwamua na hali ya maisha.
 
Nae Mkurugenzi Idara ya Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu Zanzibar bi Maimuna Fadhil Abbas amesema Idara yake itashirikiana na walimu hao ili kuliendeleza darasa hilo na litasaidia Taifa kuwa na walimu wengi wenye uwezo wa kulisoma na kulisomesha kwa umakini.
 
Aidha amesema Wanafunzi watakaopatiwa taaluma hiyo itawasaidia hapo baadae kuwa wajasiriamali wazuri ambao watakaweza kujiajiri wao wenyewe kwa asilimia kubwa badala ya kusubiri ajira kutoka Serikalini.
 
Kwa upande wao washiriki wa darasa hilo wamesema somo hilo linawasaidia sana na kuiomba Wizara kuliunga kwa kuliwezesha darasa hilo ili na walimu wengine wawe tayari kupata taaluma hiyo hali ambayo itapelekea kuwa na walimu wa kutosha wa somo hilo.
 
Pia wameitaka jamii kuondokana na mtazamo wa kuwa somo hilo ni mchezo tu, bali walipokee kwa lengo la kujenga jamii iliobora katika kutengeneza sanaa.
 
Hata hivyo bi Asya kwa niaba ya Katibu Mkuu walimu hao aliiwakabidhi baadhi ya vifaa ili viweze kuwasaidia kufanyia mazoezi kwa wanapokuwa katika darasa hilo.
 
Somo la fine art linalojumuisha kazi mbali mbali za mikono na sanaa, limeanza kusomeshwa kwa Walimu mbali mbali kutoka Skuli za Serikali na binafsi wanaendelea kujitolea kwa kengo la kujiongezea taaluma kuweza kusomesha katika Skuli zao.May be an image of 3 people, people sitting and indoorMay be an image of one or more people, people sitting and indoorMay be an image of 3 people and people sitting

Hakuna maoni